Rais wa Zambia, Edgar Lungu, anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa kwa ziara ya siku tatu, kufuatiwa na mwaliko wa Rais Dk. John Magufuli, ambapo atatembelea maeneo muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi.

Tanzania na Zambia zinatarajia kusaini mikataba minne ikiwemo ya usafirishaji ambayo kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), itasaini mkataba utakaowezesha ndege zake kufanya safari za Lusaka, Zambia.

Pia katika Ziara hiyo ya kiserikali Zambia na Tanzania zinatarajiwa kufanya maboresho ya namna bora ya ufanyaji kazi wa Tazara na Tazama, bomba ambalo lilijengwa na Julius Nyerere na Dk Kenneth Kaunda ili kuepuka vikwazo ambavyo Africa Kusini iliiwekea Zambia.

Tayari Tanzania na Zambia zimeanza mkakati wa kuboresha muundo wa TAZARA, ikiwemo kufanya mabadiliko sheria iliyounda mamlaka hiyo ili kuendana na wakati.

Video: Magufuli awatia kitanzi Gavana, bosi wa TRA, Katibu wa Fedha, CUF wachapana mbele ya jaji...
Alikiba ashinda tuzo mbili za The Nollywood & African Film Critics (NAFCA)