Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo saba vya kulelea watoto yatima kama sehemu ya kusherehekea kumbukumbuku ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 63.

Vitu hivyo, vimekabidhiwa mapema leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye piani Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega, ambaye alimwakilisha Rais Samia kukabidhi vitu mbalimbali na fedha taslimu.

”Kwa niaba ya Rais Samia tunasema shkrani sana kwa mwenye mungu lakini pia tunashukuru uongozi wa kanisa na leo ni siku maalumu ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Rais wetu, mama yetu Dkt Dkt Samia Suluhu Hassan ametimiza miaka 63,” amesema Naibu Waziri Ulega.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akikabidhi baadhi ya vitu katika kituo cha Msimbazi Center Home of Chidren .

Amesema, ”Katika furaha na bashasha yake ameona ashiriki kwenye kumtukuza na kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutoa na kutoa kwakwe ameamua kwa makusudi atoa katika vituo vya watoto yatima miongoni mwa vituo hivyo ameamua kutoa hapa katika kituo hiki cha Msimbazi Center Home of Chidren lakini na kile cha mburahati vinavyosimamiwa na Kanisa Katoliki.”

Vitu vilivyokabidhiwa, ni pamoja na pempasi za watoto, unga, sabuni, sukari, maziwa,mafuta kwa vituo vya Children home Msimbazi, Mburahati, Tua ngoma, Mbagala, Mbweni, Mwasonga na Sinza ambavyo vyote vipo jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo, limefanyika katika Kituo cha Children home Msimbazi cha Ilala jijini Dar es Salaam, pia alikabidhi zawadi hizo kwa Kituo cha Watoto Mburahati ambapo pia aliwatembelea na kujulia hali watoto hao wanaolelewa kituo hicho cha Msimbazi.

Arsenal yaipandia dau Chelsea
Morocco yaalikwa Copa America 2024