Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na ujumbe aliombatana nao ameshiriki mazungumzo na Waziri Mkuu (Premier) wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Kegiang mara baada ya kuwasili The People Great Hall, jijini Beijing nchini China.

Rais Samia ameshiriki mazungumzo hayo hii leo Novemba 3, 2022 ambapo pia alipata mapokezi ya heshima yaliyoandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China mapema baada ya kuwasili eneo hilo.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na ujumbe aliombatana nao kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa China, Li Kegiang.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu (Premier) wa Jamhuri ya Watu wa China Li Keqiang The People Great Hall, Beijing chini China.

Dkt. Mpango 'ateta' na Rais wa AfDB
Mkutano COP27 watarajiwa kuzingatia haki