Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda, G7 wanakutanahii leo (Novemba 3, 2022), kujadili namna watakavyoratibu msaada zaidi kwa Ukraine kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni, yanayofanywa na Urusi dhidi ya mifumo ya nishati yalisosababisha ukosefu wa huduma ya umeme katika maeneo mengi.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, unatarajiwa kugubika mkutano huo wa siku mbili kati ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Anthony Blinken na wenzake wa G7 mjini Muenster Magharibi mwa Ujerumani huku jukumu au ushawishi wa China duniani na maandamano yanayoendelea nchini Iran yakiwa ni mambo yatakayojadiliwa.

Moja ya mikutano ya Viongozi wa kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda, G7. Picha: Federal Ministry of Finance / Photothek

Ujerumani, ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo wa G7 na inayoshikilia urais wa kupokezana wa kundi hilo, inatoa nafasi kwa mataifa hayo tajiri duniani, kujadili zaidi kuhusu China na usalama wa eneo la Indo-Pasifiki, hasa baada ya rais Xi Jinping kupitishwa kuongoza kwa muhula wa tatu madarakani katika mkutano wa chama chake tawala cha kikomunisti.

Haya yanajiri ikiwa tayari Viongozi wa kiarabu wamekuwa makini kutochukua msimamo katika vita vya Urusi nchini Ukraine, na badala yake wakitoa wito wa suluhu ya kisiasa katika mgogoro huo unaoyumbisha uchumi wa mataifa mengi duniani.

Serikali yasitisha zoezi Hereni za kielektoniki
Kiongozi Young Africans aungana na mashabiki