Klabu ya soka ya Antalyaspor ya nchini Uturuki imemjumuisha kikosini mshambuliaji wake Samuel Eto’o katika mchezo unafouata dhidi ya Galatasaray hii ikiwa ni kinyume na matarajio ya wengi.

Mwenyekiti wa Antalyaspor Ali Safak Ozturk amesema kuwa Eto’o ameomba radhi na mwenye moyo mgumu mithili ya jiwe linalokaa majini na haliingii maji ndio anapaswa kutokumsahe.

”Tunatumai atajirekebisha na atakuwa na mchango mkubwa katika timu yetu”Ozturk amekiambia kikosi cha timu hiyo.

Hivi karibuni mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon aliwekwa nje ya kikosi kutokana na kutoa maneno ya kibaguzi kwa uongozi wa klabu hiyo aliyoyaweka katika mtandao wake wa Instagram akisema kuwa ”Yamkini baadhi ya watu hawaniheshimu kwa sababu mimi ni mweusi”

 

Rigobert Song Yu Hoi, Akimbizwa Hospitali
Arsene Wenger: Sikuona Kama Ameshika Ama Hakushika