Serikali imepiga marufuku mifuko ya plastiki inayotumika kufungashia pombe kali zinazopatikana kwa bei nafuu maarufu kama viroba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba alisema kuwa sambamba na hilo Serikali imepiga marufuku uingizwaji na utengenezaji wa mifuko yote ya plastic kuanzia mwaka ujao.

Alisema kuwa mifuko hiyo ya plastic inayotolewa bure kama vifungashio imekuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa. Alisema mifuko hiyo inachangia pia katika kuziba mifereji na kusababisha mafuriko wakati wa mvua kubwa.

“Tumeamua kutangaza ili kuwaandaa wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu mwingine utakaowekwa na serikali. Asilimia ya uchafu kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastic,” alisema Makamba.

Baadhi ya wafanyabiashara kwenye maduka ya bidhaa mbalimbali zinazofungashiwa kwenye mifuko hiyo, walishauri Serikali kutafuta njia mbadala mapema kwa ajili ya vifungashio.

“Tangu wameamua kupiga marufuku sio leo, labda safari hiii wameamua kweli… ngoja tuone,” alisema Jamal Hamsini, mmiliki wa duka la nguo katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Kocha wa Pacquiao atosa ombi la Mayweather licha ya kumtamanisha kwa mamilioni
Kiongozi wa Upinzani ashambuliwa, uso wafurika misosi

Comments

comments