Naibu waziri wa elimu, sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya alizungumza bungeni kuhusiana na ongezeko la fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanahifadhiwa na bodi ya mikopo litatimilika baada ya utafiti utaofanyika ndani ya miaka miwili kubaini gharama halisi za chakula na malazi kwa wanafunzi.

Ufafanuzi huo ulitolewa kufuatiwa na swali la mbunge wa viti maalumu, Zainabu Katimba (CCM) aliyehoji kuhusu na ongezeko la fedha kwa wanafunzi kutoka sh8,500 hadi sh10,000 kwa madai kuwa gharama za maisha zimepanda.

“Ongezeko hilo haliendani na kasi ya mfumuko wa bei uliorekodiwa na ofisi ya taifa ya Takwimu (NBS) Kutoka asilimia 4.2 Februari 2016 hadi kufikia asilimia 5.6 Februari 2016,” alisema Katimba. Pia aliendelea kwa kusema 2015/16 bodi ya mikopo ilifanya ongezeko la fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sh1,000 kutoka sh7,500 hadi kufikia sh8,500.

Wananchi wamkubali JPM, Twaweza watoa matokeo utafiti 'Rais wa Watu?....'
Audio: Lowassa - Magufuli anafanya vizuri, Asema CCM inafanya vizuri zaidi vjijijni kuliko Upinzani