Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy ameituhumu Urusi kwa vitendo vyake vya kigaidi na mauaji nchini Ukraine, baada ya shambulio moja kuleta madhara katika wodi ya wazazi na kuuwa kichanga katika mkoa wa kusini, wa Zaporizhzhia.

Maelezo ya mashuhuda na Waokoaji yamesema, mtoto huyo mchanga ameuawa usiku wa kuamkia leo (Novemba 24, 2022), kufuatia shambulio la roketi dhidi ya hospitali katika mji wa Vilniansk, ambapo jengo la ghorofa mbili la wodi ya wazazi liliharibiwa.

Sehemu ya uharibifu uliofanyika katika moja ya jengo la uzazi nchini Ukraine. Picha ya WBFF.

Aidha, inaarifiwa kuwa Mama wa mtoto huyo na Daktari waliondolewa wakiwa hai huku Gavana wa mkoa huo akisema roketi zilizofyatuliwa na kushambulia zilikuwa ni za Urusi.

Shambulio hilo, linaongeza mateso yalioshuhudiwa katika hospitali na vituo vingine vingine vya matibabu ambalo limeleta athari kwa wagonjwa, wafanyakazi na raia kufuatia mashambulizi hayo yanayoingia mwezi wa tisa wiki hii.

Uongozi Simba SC washauriwa Dirisha Dogo
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 24, 2022