Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Isaac Njenga kuhusu ushirikiano wa Mataifa hayo mawili katika sekta ya umeme na Gesi.

Wakiwa katika Mkutano huo, Waziri Makamba amemueleza Balozi Njenga kuwa Tanzania ipo tayari kuendeleza ushirikiano na Kenya katika Sekta ya Gesi na Umeme kutokana na nchi hizo kuwa na mahusiano mbalimbali ya kisekta.

Waziri wa Nishati, January Makamba.

Akizungumzia mradi wa usafirishaji Gesi kutoka Tanzania kwenda Kenya, Makamba amesema mradi huo ni kipaumbele cha Viongozi Wakuu wa pande hizo mbili na tayari timu za majadilino kutoka Kenya na Tanzania zinaendelea na kazi ya uandaaji nyaraka.

Kwa upande wake, Balozi Isaac Njenga amesema Kenya ipo tayari kutekeleza makubaliano ya ushirikiano yaliyoingiwa kwenye mradi wa usafirishaji gesi kutoka Tanzania na usafirishaji wa umeme kwa msongo wa KV 400 ambao utaziwezesha Tanzania na Kenya kuuziana umeme.

Leandro Trossard kupima afya London
Morrison, Aziz Ki wabanwa Young Africans