Klabu ya Arsenal ipo katika mipango ya mwisho ya kumsainisha mkataba mpya kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil.

Gazeti la The Daily Mirror la nchini England limeripoti kuwa, uongozi wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London umeandaa mkataba wa muda mrefu ambao utamuwezesha Ozil kulipwa mshahara wa Pauni laki mbili (200,000) kwa juma.

Kwa sasa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vyema na hadi kufikia kipindi hiki cha michezo ya kimataifa kwa timu za mataifa mbali mbali duniani, mambo yameripotiwa kuwa katika mustakabali mzuri.

Ozil, mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa anaendelea na mkataba aliousaini miaka mitatu iliyopita akitokea Real Madrid ambao unamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni laki moja na arobaini (140,000) kwa juma.

Mkataba wa sasa wa kiungo huyo umesaliwa na miezi kumi na nane (18) ambayo ni sawa na mwaka mmoja na nusu.

Taarifa nyingine kutoka kaskazini mwa jijini London zinaeleza kuwa, mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez, naye anakaribia kusaini mkataba mpya.

CCM yatuhumiwa kuuza shule kinyemela, yadai elimu bure imechangia
Usain Bolt Kutua Signal Iduna Park Majira Ya Kiangazi