Aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa anafahamu kuwa Tundu Lissu anayo mengi ya kuzungumza juu ya tukio la kupigwa risasi kwani gari lililotumika na washambuliaji ndilo gari ambalo baadhi ya wabunge walidai linawafuatilia.

Amesema kuwa ingawa vyombo vya dola vitaendelea na kazi ya upelelezi lakini angependa kama Lissu akirudi kutoka kwenye matibabu azungumzie zaidi kwani hata siku alipozungumza na wanahabari kuhusu gari linalomfuatilia hakusema kwa undani.

“Mh. Lissu pamoja na dereva wake ninauhakika wana mengi ya kusimulia juu ya hili kwani tangu amelilalamikia siyo muda mrefu kutoka sasa. Na kwa vile tayari amejeruhiwa anaweza akatueleza kwa kina juu ya tukio hili,”amesema Nape

Hata hivyo, Nape ameongeza kuwa gari hilo limeripotiwa kuwafuatilia wabunge kadhaa akiwemo yeye na walisharipoti gari hilo kuwa hawalielewi ni mtu gani anayewafuatiliaga na kuongeza kuwa namba za gari hilo ni zile zile na idadi ya watu ni hao hao lakini hatua hazijachukuliwa.

 

Video: Tundu Lissu dunia nzima, Vigogo waanza kukamatwa
Mayay aahidi kufanya makubwa TFF