Pengine yaliyomkuta mwanamuziki wa marekani Chris Brown baada ya kumtembezea kichapo aliyekuwa mpenzi  wake wakati huo Rihana, yanaweza yakajirudia kwa rafiki yake wa karibu Micheal Ray Nguyen-Stevenson maarufu Tyga.


Hii ni baada ya kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kumpiga na kumsababishia majeraha kadhaa mwilini mpenzi wake wa zamani Camaryn Swanso ambapo inaelezwa kuwa mrembo huyo alitembelea nyumbani kwa  rapa Tyga siku ya jumatatu oktoba 11, 2021 majira ya saa tisa usiku, mahala ambapo awali alikatazwa kabisa kufika.


Taarifa za awali zinasema kwamba mrembo huyo Camaryn Swanso alikuwa amelewa sana, na kuwa licha ya hali hiyo Rapa Tyga alimruhusu kuingia  ndani kwa ajili ya mazungumzo  naye na baadaye zilianza kusikika kelele za Camaryn ambaye amelieza jeshi la polisi kwamba Tyga alikuwa akimrushia ngumi wakati wa majibizano yao. 

Mama mzazi wa Camaryn alifika katika nyumba hiyo na kumchukua na kisha kuwa taarifu polisi kuhusu tukio hilo.kwa mujibu wa TMZ, Polisi walifika nyumbani kwa Tyga usiku huo kwa ajili ya uchunguzi wa mwanzo ambapo Rapa Tyga pia  ameripotiwa kufika kutoa maelezo kwa upande wake ikiwa tayari amefunguliwa kesi ya unyanyasaji

Mfikirwa afichua mpango Young Africans
Morrison aandaliwa mkakati maalum Botswana