Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kushtukiza kukagua awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi unaofanyika kutoka eneo la Kariakoo hadi Mbagala, katika eneo la Mtoni Mtongani mkoani Dar es salaam na kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo, ambao kwa sasa umefikia asilimia 16.

Akizungumza na Wakazi wa eneo hilo mara baada ya ukaguzi huo, Rais Samia amesema serikali itahakikisha ujenzi wa barabara hiyo unakamilika katika muda uliopangwa ili kuwarahisishia usafiri wakazi wa maeneo hayo.

Amesema Serikali itashughulikia changamoto zote ambazo zitaonekana kuwa ni kikwazo katika ujenzi wa barabara hiyo.

Rais Samia ameahidi kurejea katika eneo hilo  siku chanche zijazo, kwa lengo la kukagua tena maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.

Ujenzi wa mradi huo awamu ya pili kutoka Gerezani Mpaka Mbagala ulionza mwaka 2019, ni mradi unaogharimu kiasi cha shilingi billioni 200, Mradi wa mwendokasi ni wenye awamu sita za ujenzi ambao unaweza kwenda zaidi ya miaka kumi.

Polisi Tanzania waitishia Simba SC
Kocha Gomes afichua siri Simba SC