Wakuu wa Wilaya nchini wametakiwa kuweka ajenda ya mazingira kama kipaumbele katika maeneo yao na kubuni mikakati endelevu ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni, ili kasi ya ukataji wa miti kwa ajili ya kupata nishati hiyo ya kupikia iweze kupungua.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo wakati akiwasilisha vipaumbele vya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Wakuu wa Wilaya, ili kuwajengea uelewa utakaowasaidia kusimamia utekelezaji katika maeneo yao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha vipaumbele vya Ofisi ya Makamu wa Rais kwawakuu wa wilaya ili kuwajengea uelewa utakaowasaidia kusimamia utekelezaji wa vipaumbele vinavyotekelezwa katika maeneo yao ya utawala, wakati wa kikao kazi cha viongozi hao kilichofanyika jijini Dodoma.

Amesema, Viongozi hao pia wanatakiwa kuendelea kusimamia vyema zoezi la upandaji wa miti milioni 1.5 kwa kila halmashauri na kuwapongeza kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha kuwa mazingira yanahifadhiwa, kuwa endelevu na kusimamia vyema zoezi la upandaji miti.

“Ndugu zangu tangu tuzindue Kampeni Kabambe ya Hifaddi na Usafi wa Mazingira tarehe tano mwezi wa sita mwaka 2021, ninyi wakuu wa wilaya mmekuwa mkisimamia ipasavyo kampeni hii kwa kuhamasisha upandaji wa miti, mmemuheshimisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema.

Sehemu ya wakuu wa wilaya nchini wakiwa katika kikao kazi cha kusikiliza vipaumbele vya wizara mbalimbali vipaumbele vinavyotekelezwa katika maeneo yao ya utawala, wakati wa kikao kazi cha viongozi hao kilichofanyika jijini Dodoma.

Uwasilishaji wa vipaumbele hivyo, unatokana na maombi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ya kuwataka wakuu hao kupitishwa kwenye utekelezaji wa shughuli za Wizara za kisekta, ili kwenda kusimamia na kutekeleza majukumu hayo kwa weledi.

Ujenzi Kiwanda cha Saruji kuibua fursa kiuchumi Dodoma
Nahodha Horoya AC: Tutaishangaza Simba