Wizara ya Afya nchini, inatarajia kuzindua dozi ya nyongeza ya Uviko-19 (Booster), ambayo itatolewa kwa hiari ili Wananchi waweze kuongeza kinga zaidi dhidi ya ugonjwa huo.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Afya kwa kipindi cha Julai – Desemba 2022, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Amesema, ndani ya kipindi hicho Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya walifanikisha utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko-19 kwa kufikia asilimia 86 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2022 jumla ya dozi 46,848,520 zilikuwa zimepokelewa na dozi 41,581,670 zilisambazwa nchi nzima, huku kiasi cha chanjo zilizosalia kwenye bohari ya kutunzia ni 5,266,850 aina ya JJ.

Morrison, Aziz Ki wabanwa Young Africans
Mangungu afichua lilipo basi la Simba SC