Rais John Magufuli amemuapisha Balozi Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan mapema leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jana, Rais Magufuli alitangaza uteuzi wa Balozi Chikawe, ambapo Balozi huyo atakuwa na jukumu la kidiplomasia katika nchi hiyo ambayo imekuwa rafiki wa karibu wa kimaendeleo na Tanzania.