Takriban Wafugaji 27 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika eneo lenye mivutano ya kikabila na kidini nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa Kamishna wa polisi wa Nasarawa, Maiyaki Muhammed Baba amesema Wafugaji hao, ambao walikuwa wakichunga mifugo, walikuwa katika kijiji cha Rukubi kilichopo kwenye mpaka kati ya majimbo ya Nasarawa na Benue.

Moja kati ya matukio ya mauaji ambayo yaliwahi kutokea nchini Nigeria. Picha ya The Telegraph.

Amesema, “Tumegundua watu 27 waliuawa katika mlipuko wa bomu pamoja na ng’ombe kadhaa, alisema na watu wengi walijeruhiwa na idadi ya vifo inaweza kuongezeka na tayari wataalam wa mabomu wameanza kuchunguza chanzo cha mlipuko huo.”

Chama kinachowakilisha wafugaji, kimesema mlipuko huo ulisababishwa na shambulizi la anga la kijeshi, huku kukiwa hakuna taarifa za kundo lolote la uasi lililodai kuhusika na shambulio hilo lililoacha simanzi na vilio kwa jamaa za marehemu.

Mtuhumiwa wa ulawiti Wanafunzi 18 mikononi mwa Polisi
Wadakwa na kilo 399 za bangi, silaha