Wakala wa majengo Tanzania (TBA) wameanza kutimiza ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa wananchi kwa kuanza ujenzi wa miradi ya nyumba za watumishi wa umma bunju na mradi mwingine uliopo magomeni kota.

Ahadi hiyo imeanza kutimia mara baada Makonda kufanya ziara ya kukagua miradi hiyo ya Ujenzi inayosimamiwa na Wakala wa Majengo  Tanzania (TBA) na kujionea shughuli mbalimbali  zinavyoendelea, miradi aliyoitembelea ni pamoja na ule wa Bunju  unaojengwa nyumba za watumishi wa umma kwa Mkoa wa Dar es salaam, pia Mradi wa Magomeni kota.

Makonda ameipongeza Wakala wa Majengo Tanzania kwa hatua waliyofikia katika ujenzi huo na kuongeza kuwa miradi hiyo itakuwa mkombozi kwa  watumishi wa umma.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Elius Mwakalinga amesema mradi huo utakuwa na nyumba 851 ambazo zitajengwa  na mpaka sasa tayari wameshajenga nyumba 219. Amesema ndani ya wiki mbili zijazo wataanza kujenga nyumba zingine 300 katika mradi huo wa Bunju, ameongeza kuwa kufikia mwezi Januari mwakani wataanza kujenga maghorofa katika mradi wa Magomeni kota.

Hata hivyo mwakalinga amesema kuna awamu inayofuata niwatajenga nyumba kwa fedha za TBA na kuwapangisha watumishi wengine katika eneo hilo la magomeni kota.na kuongeza kuwa kuna mikoa kumi na tisa ambayo wanajenga nyumba tatu tatu na kwa mkoa wa dodoma watajenga nyumba miamoja na kufikia mwisho wa mwezi huu mradi huo utaanza.

Chadema yashinda Umeya Manispaa ya Ubungo
Rais Magufuli azindua barabara ya mchepuko jijini Nairobi