Jumla ya watoto milioni 1.3 ambao ni sawa na asilimia 115 wamepata chanjo ya Polio ikiwa ni moja ya lengo la kufikia watoto 975,839 la kuwapatia chanjo kwa awamu ya kwanza huku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiwataka wazazi na walezi wenye watoto kuhakikisha wanapata kinga hiyo.

Afisa Programu Mpango wa Taifa wa chanjo kutoka Wizara ya Afya, Lotalis Gadau ameyasema hayo jijini Dodoma na kudai kuwa kampeni hiyo ilihusisha mikoa ya Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe huku awamu ya pili ikiwafikia watoto milioni 12.1 na kuvuka lengo lililowekwa la kuwafikia watoto milioni 10.2 .

Amesema, awamu hii ya tatu ya chanjo ya polio imelenga kuwafikia watoto milioni 12.3 wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima, na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akisema zoezi hilo litawalenga watoto walio na umri chini ya miaka mitano.

“Shughuli ya utoaji chanjo mkoani hapa (Dodoma) imefanyika kwa siku nne ikilenga kampeni ya nyumba kwa nyumba hivyo wazazi hawakuwa na sababu ya kuwabeba watoto na kuwapeleka vituoni kwa ajili ya kupata chanjo hiyo ambapo wahudumu wa afya walipita majumbani kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo ya matone kwa watoto.” alifafanua Senyamule.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliasa kuwa, “Watoto wote wachanjwe asibaki mtoto hata mmoja ambaye hajapata chanjo, kwa kufanya hivi tutakuwa tumewaokoa watoto wetu dhidi ya mateso ya ugonjwa wa polio.”

Awali, mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma, Francis Bujiku alisema, mkoa huo unatarajia kuwafikia watoto walio na umri chini ya miaka mitano wapatao 591,624 na kuidai kuwa wazazi na walezi bado wanayo nafasi ya kuhakikisha watoto wanapata chanjo hiyo pindi wanapoenda kliniki au kituo chochote cha kutolea huduma za afya.

Serikali 'yawabana koo' Wakandarasi ujenzi miradi ya Maji
Kipanga FC kuifuata Hilah FC Wau Dar es salaam