Sheria ya kulinda taarifa binafsi za kimtandao, imepata kibali ambapo sasa Baraza la Mawaziri linatarajia kukaa na kuijadili ili kuwasilisha muswada huo Bungeni Septemba 13, 2022.

Hayo, yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kongamano la siku mbili lililowakutanisha wadau wa Teknolojia ya habari na mawasiliano toka nchi mbalimbali barani Afrika.

Amesema, muswada huo utapelekwa bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kuanza kujadiliwa na kukamilika kwake kutasaidia taarifa za watu binafsi kutotoka nje.

Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

“Baraza la Mawaziri limeshaandaa muswada wa sheria hiyo ili kuondoa tatizo la baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao na baada ya muswada huu kupelekwa bungeni, kila mdau atatakiwa kutoa maoni yake,” amefafanua Waziri Nape.

Aidha, ameongeza kuwa kongamano hilo litaelimisha mambo mbalimbali ya TEHAMA ili kubadilishana uzoefu wa wadau sekta hiyo wakiwemo wa miundombinu kutoka ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa, “Lengo la Serikali halitaki kumwacha nyuma mtanzania kwa kuwa teknolojia ya kisasa itasaidia mambo mengi ikiwemo kwenye ajira na hata kupata wawekezaji wengi.”

Wadau wa Habari katika moja ya majadiliano katika warsha iliyoandaliwa na MISA Tanzania, jijini Dodoma.

Wadau mbalimbali wakiwemo watunga Sera, Wadhibiti, Watoa Huduma na wawekezaji huduma za mawasiliano wameshiriki mkutano huo ili kuzijadili na kuzifanyia tathmini ajenda za Kitaifa za Maendeleo.

Kipanga FC kuifuata Hilah FC Wau Dar es salaam
PICHA: Kikosi cha Simba SC chawasili Lilongwe