Polisi katika mji mkuu wa Marekani, wametoa taarifa za vifo vya watu wawili Donna Mueller (75), na James Mueller (76), na wengine wawili kuwa katika hali mahututi baada ya kupigwa na radi eneo lililo karibu na Ikulu ya ya Marekani usiku Agosti 5, 2022.

Taarifa ya Polisi, kutoka idara ya zima moto na dharura ya Washington ilisema radi hiyo ilipiga eneo la Lafayette Square, katika bustani ndogo iliyo kando ya barabara kutoka Ikulu ya White House, muda mfupi kabla ya saa 7:00 jioni.

Miili na majeruhi wa tukio hilo, wote walipelekwa katika hospitali za mitaa, huku Polisi wa Metropolitan wakithibitisha kwamba watu wawili waliofariki walikuwa ni wakazi wa eneo la Janesville lililopo Wisconsin.

Msemaji wa Ikulu ya White House na Katibu wa Vyombo vya Habari, Karine Jean-Pierre wamesema Rais Joe Biden amehuzunishwa na vifo vya watu waliopoteza maisha, na kuwaombea afya njema majeruhi ambao bado wako katika hali mbaya.

Dhamira ya Rais sekta ya Kilimo kuleta mabadiliko kiuchumi
PPRA yafunguka fursa zaidi ya sh. 6 trilioni kwa makundi maalum