Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amezindua Bodi ya Shirika la Mzinga lililopo Mkoani Morogoro na kuitaka kuweka utaratibu wa kutambua juhudi za Wafanyakazi katika idara na vitengo mbalimbali shirikani.

Akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, Waziri Bashungwa amewapongeza Wajumbe walioteuliwa na kusema ana imani kuwa watatoa mchango mkubwa, ili kufikia malengo ya Serikali huku akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi, Luteni Jenerali Samweli Ndomba (Mstaafu), kwa kuendelea kuaminiwa na kuteuliwa kwa mara nyingine na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Mkoani Morogoro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Luteni Jenerali Samweli Ndomba (Mstaafu), alimweleza Waziri Bashungwa kuwa, Mzinga ni Shirika la Kimkakati litakaloendelea kutimiza majukumu yake ya msingi pamoja na kuongeza ubunifu katika teknolojia na kuongeza wigo wa kuzalisha mazao ya aina tofauti tofauti.

Katika zoezi hilo, Meneja Mkuu na Katibu wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Brigedia Jenerali Hamisi amesema uzinduzi wa Bodi hiyo utasukuma gurudumu la maendeleo ya Shirika la Mzinga na kufanikisha azma na Serikali.

Waamuzi Simba SC, Young Africa watajwa
PICHA: Young Africans yaondoka Dar es salaam