Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amezungumiza kifo cha Mtanzania, Nemes Tarimo aliyefariki dunia nchini Urusi akisema kijana huyo alikwenda nchini humo mwaka 2020 kujiunga na Chuo Kikuu cha Moscow Technological University (MIREA), kwa masomo ya Shahada ya Uzamili fani ya Business Informatics.

Dkt. Tax, ambaye alikuwa akizungumza na Waandhish wa Habari katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam amesema Tarimo akiwa masomoni mwezi Machi 2022 Tarimo alitiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu na kuhukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax wakati alipiokuwa akizungumza na Waandishi wa habari.

Amesema, akiwa gerezani Tarimo alijiunga na kikundi cha kijeshi cha Urusi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha na kuachiwa huru baada ya vita kumalizika na alifikwa na umauti akiwa katika uwanja wa vita tarehe Oktoba 24, 2022.

Aidha, Dkt. Tax ameongeza kuwa mwili wa marehemu umeondoka nchini Urusi tarehe Januari 24, 2023 na unatarajiwa kuwasili nchini muda wowote na kuongeza kuwa wamekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Urusi, ili kuhakikisha mwili wa Marehemu Tarimo unarejeshwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kiwango cha Metacha chamkuna Nabi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 25, 2023