Zlatan Ibrahimovic ametoa maneno ya kejili kwa wafaransa, kwa kujivunia kiwango chake cha soka alichokionyesha kwa muda wa miaka mitatu akiwa na klabu bingwa nchini Ufaransa, Paris St Germain.

Zlatan, amesema kiwango chake kimekua chachu kubwa ya kupandisha soka la nchini Ufaransa upande wa klabu za soka nchini humo, kutokana na kuiwezesha PSG kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Zlatan ametoa maneno hayo, alipohojiwa na baadhi ya waandishi wa habari akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Sweden kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya mtoano wa kuwania kufuzu fainali za Ulaya za mwaka 2016 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Denmark.

Amesema mchango wake ambao umekua ukiisaidia PSG, hauna budi kushukuriwa na mashabiki wa soka nchini humo, kutokana na kutambua kwamba ni kipindi cha muda mrefu klabu za Ufaransa zilikua hazifanyi vyema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ameongeza kwamba wakati wote alijiwekea dhamira ya kucheza soka nchini Ufaransa, na alifanikisha kutimiza ndoto hizo mwaka 2012 aliposajiliwa na PSG, akitokea AC Milan nchini Italia.

Hata hivyo amewataka baadhi ya mashabiki kutomuelewa vibaya kwa kauli aliyoitoa, kwa kudhani huenda ikapokelewa tofauti na alivyokua akimaanisha.

Mpaka sasa Zlatan Ibrahimovic, ameshacheza michezo 99 akiwa na klabu ya PSG na kufunga mabao 84.

Lowassa: Hili Muulizeni Magufuli
Roy Hodgson Afichua Siri Nzito