Lydia Mollel – Morogoro.

Ujenzi wa jengo la Wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa umekuwa chini ya viwango, huku gharama ya ujenzi huo ikikadiriwa kuwa ni Shilingi milioni 280 kutoka Serikali kuu, jambo ambalo limemshitua Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaka Hamdu Shaka ambaye ameagiza uchunguzi kufanyika.

Dc Shaka,ameonyesha kushangazwa na ubora duni wa vifaa na ujenzi, akitolea mfano wa matumizi ya vifaa vya vilivyo na mapungufu na kutokuwepo kwa ubora unaotakiwa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Saimon Swai ameelezea changamoto ya kutopatikana kwa mkandarasi wa awali, hivyo ujenzi kulazimika kuanza upya na mkandarasi mpya kwa kutumia fedha za hospitali.

Hata hivyo, Shaka amesisitiza kuwa watakaobainika kuhusika na uzembe watapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria, na ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha hilo linatekelezwa.

Kipato cha Mwanamke: Mradi mazao ya uvuvi wazinduliwa
Yao Kouassi kuikosa Mamelodi Sundowns