Kiungo kutoka nchini Uturuki Arda Turan amefichua siri za kukataliwa kuachana na FC Barcelona, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi ambao ulifungwa rasmi mwishoni mwa Agosti mwaka huu.

Turan ambaye alionekana kupoteza muelekeo wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha FC Barcelona tangu aliposajiliwa mwaka 2015 akitokea Atlético Madrid amesema tayari dau la Euro milion 50 lilikua limeshawasilishwa Camp Nou na uongozi wa klabu ya Jiangsu Suning ya nchini China lakini ombi hilo lilikataliwa.

Klabu ya Jiangsu Suning ilituma ofa hiyo huku ikiwa tayari imeshafanikiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa barani Ulaya kama Jackson Martinez, Ramires, Hulk pamoja na Alex Teixeira.

Akizungumza na televisheni ya Beyaz TV, Turan alisema kutua kwa ofa hiyo klabuni hapo kulimuaminisha huenda angeondoka na kwenda kusaka maisha mashariki ya mbali, lakini uwepo wa jina lake katika mipango ya meneja Luis Enrique ilikwamisha kabisa mchakato huo.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 ameongeza kuwa, kuzuiliwa kwa mpango wa kuondoka kwake Camp Nou aliupokea kama sehemu ya kuendelea na changamoto zilizokua zinamkabnili tangu alipowasili klabuni hapo na anaamini hatua hiyo ilimjenga na kufikia hatua ya kuaminiwa.

Joseph Omog Amuweka Chini Kichuya Na Kumpa Wosia
Tostao: Neymar Atakabidhiwa Kombe La Dunia 2018