Msaniii Bob Junior, amesema kutokufanya vizuri kwenye muziki wa Bongo fleva kwa kipindi cha miaka miwili iliyo pita ni kutokana na kusumbuliwa na maswala ya kifamilia,

Bob amesema kwa kipindi chote alichokuwa hafanyi vizuri alikuwa anamuuguza mama yake mzazi, hivyo alishindwa kuwekeza muda wa kutosha kwenye kusimamia kazi zake za muziki

Akizungumza na Times FM, mwimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki amesema hakuwa makini na masuala ya muziki ili kutatua na matatizo ya familia yake.

“Sikuwa serious (makini/kumaanisha) kwenye muziki kwa sababu mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia. So, ilibidi niweke nguvu kwenye masuala ya familia, kumlea mama yangu. Hii ndiyo sababu kwa mwaka mmoja na nusu Bob Junior hakuwa serious na muziki,” alisema.

Msanii huyo ambaye  ameachia wimbo mpya “Give me “amesema hivi sasa amejipanga kurudisha heshima yake kwenye muziki wa Bongo flava na atakuwa akitoa nyimbo mara kwa mara.

Video: Hivi ndivyo Lukaku alivyoiliza Everton
Tisa wakamatwa kwa kuwabaka waumini kwenye ibada za mkesha