Nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, John Bocco ameibuka kwenye mitandao ya kijamii na kutoa shukurani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji ‘Mo’.

Bocco ametoa shukurani hizo kwa kuweka picha ya Ubingwa wa Ligi Kuu ambao alikabidhiwa Julai 18, Uwanja wa Benjamin Mkapa na kisha kumkabidhi ‘Mo’.

Hata hivyo maelezo yaliyoandikwa na Mshambuliaji huyo aliyemaliza msimu kwa kuongoza orodha ya wapachipa mabao msimu wa 2020/21, yameleta ukakasi kufuatia kinachoendelea kati ya Haji Manara na baadhi ya viongozi wa Simba SC.

Bocco ameandika: Ulistahili kupokea hii zawadi @moodewji ukiwa kama mwenyekiti wetu na muwakilishi wa wanasimba wote @simbasctanzania niwashukuru mashabiki wetu kwa umoja wenu na upendo kwa sisi wachezaji wenu.

Niwashukuru sana viongozi wetu kwa juhudi maarifa na mazingira mazuri wanayotuwekea sisi wachezaji ilikuifanya kazi yetu vizuri @bvrbvra, @moodewji pokea asante yetu boss tunathami sana moyo wako na mazingira mazuri ya kazi unayotuwekea boss pamoja na bodi yako kwa ujumla.

@simbasctanzania umoja wetu na upendo wetu ndio nguzo ya sisi kufanya vizuri zaidi kwa msimu unaokuja ni wakati wakuzidisha imani, upendo na umoja kwa wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi wetu ili tuzidi kupata mafanikio makubwa zaidi kwa misimu ijayo.

@hajismanara nikushukuru kaka kwa kuitumikia club yetu nakutakia kheri kwa kila jambo kaka mkubwa.

Nnguvu Moja.

TBS imeiingizia serikali bilioni 3.9 ukaguzi wa magari
Kesi ya Mbowe yahairishwa kisa mtandao