Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka tisa katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama mtoto huyo aliokota bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha kulipukiwa.

“Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba, kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28, mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota Bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kulipuka na kusababisha apoteze maisha”,amesema Kamanda Manyama.

Polisi inahusisha uwepo wa Bomu hilo katika kijiji hicho kuwa huenda lilikuwa likitumiwa kama njia na makundi ya waasi waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda kambi ya wakimbizi ya Mtabila hivyo kudhaniwa huenda liliangushwa na watu hao.

Jeshi la polisi limetoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea

Wanne bandari mikononi mwa TAKUKURU
Drone kuruka kwa dola 100