Meneja wa Klabu ya AC Milan, Stefano Pioli, amesema ana furaha kufanya kazi na Brahim Diaz ambaye hatma yake ya kusalia klabuni hapo itajulikana mwishoni mwa msimu huu.

Diaz amekuwa akicheza ndani ya Milan kwa mkopo akitokea Real Madrid, muda wake huo wa mkopo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu akicheza hapo kwa msimu wa pili.

Nyota huyo inaelezwa klabu yake ya Madrid inataka kumuongezea mkataba, lakini haijaweka wazi kama itamrejesha kikosini hapo.

Pioli amesema: “Brahim Diaz najua ni mchezaji wa Real Madrid, ni mchezaji aliyekamilika, nina furaha kufanya naye kazi, mwenyewe ana furaha kuwa hapa, lakini tutaangalia mambo yatakuwaje.

“Suala la kununuliwa au kuendelea kucheza kwa mkopo wakati ukifika itajulikana ila kwa sasa anaipambania timu yake hii kufanya vizuri.”

Kocha Namungo FC bado anashangaa
Mwinyi Zahera: Hatujakata tamaa, tutapambana