Mwanamuziki mahiri wa RNB kutoka nchini Marekani Christopher Maurice Brown maarufu Chris Brown amewatolea povu zito watu wanaondelea kumshutumu kutokana na tukio la ugomvi uliotokea mwaka 2009 baina yake na aliyekuwa mpenzi wake mwimbaji Rihanna, ambapo nyota huyo alimtembezea kichapo.

Kitendo kilichoibua gumzo kubwa kote ulimwenguni na hata kupelekea kuachana kwa wawili hao, ambao mahusiano yao yalikuwa yakifuatiliwa na idadi kubwa ya mashabiki wao duniani.

Chris Brown amedhihirisha kutoridhishwa kiasi cha kuvunja ukimya na kuwataka wanaoendelea kumchukia na kuzungumza vibaya kuhusu tukio hilo kuacha mara moja kwa kuwa muda umepita na hata hivyo wakati anafanya tukio hilo alikuwa na umri wa miaka kumi na saba (17).

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Insta Story) Brown amesema kuwa kwa sasa amefikia umri wa miaka thelathini na na tatu (33) na tukio lilinalozungunzwa lilitokea takriban miaka 14 iliyopita, kwa hivyo amechoka kuwavumilia wanaondelea na kujadili suala hilo hasa katika mlengo wa kumkandamiza na kumfanya kuonekana mkosaji.

“Kama ninyi wote bado mnanichukia kwa kosa nililolifanya nikiwa na umri wa miaka kumi na saba, tafadhalini, kwa sasa nina miaka thelathini na tatu, nimechoshwa na wote mnaoendelea kulizungumzia suala hili.

Ninyi ndio wale mnaotulia kila wiki kutazama Blueface na Chrisean wakipigana dunia nzima ikitazama, hilo ni sawa? Ni la kuburudisha?” Ameandika Brown.

Harmonize afunguka siri nzito, Burna Boy na Davido

Mchungaji Kimaro wa KKKT apewa msamaha
Odinga: Tunarudi enzi za chama kimoja 'Mtukufu Rais'