Mabingwa wa soka nchini England, klabu ya Chelsea huenda ikawa imepata nguvu ya kupambana katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, dhidi ya Paris Saint-Germain, kufuatia uhakika uliotolewa na mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Diego Costa wa kuwa tayari kupambana hii leo.

Costa, alikosa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo Chelsea walibanwa mbavu na Stoke City katika ligi ya nchini Engalnd, kufuatia maumivu ya nyama za chini ya bega ambayo yalikua yakimsumbua.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amedai kuwa fit kuwavaa PSG na huenda meneja wa muda wa The Blues, Guus Hiddink akampa nafasi ya kuanza ama kumtumia kama mchezaji wa akiba kutokana na atakavyoona umuhimu wake katika mpambano wa leo.

Lakini mpaka sasa bado haijaelezwa kama moja ya njia hizo mbili itakayoanza kutumia ni ipi, ila kuna uhakika kwa Diego Costa akacheza dhidi ya PSG ambao wanaongoza kwa mabao mawili kwa moja.

Wakati Costa akitarajia kurejeshwa uwanjani hii leo, beki wa PSG, David Luiz ameahidi kupambana nae kwa udi na uvumba ili kuhakikisha hawaletei madhara katika lango lao.

Luiz amesema Diego ni rafiki wake wa karibu, lakini linapokua suala la kupambana uwanjani kwa maslahi ya klabu zao, jambo ya ukaribu wao huwa linakua mbali na kazi na chochote kinaweza kutokea.

Amedai kwamba mara nyingi Diego, hapendi kuguswa wala kukabwa kama ilivyo kwa washambuliaji wengine, lakini yeye kama mlinzi wa PSG, huwa hajali hilo na badala yake hutimiza majukumu yake ipasavyo.

Msimu uliopita wakati PSG wakipambana na Chelsea katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, wawili hao walipaniana vilivyo na ilifikia wakati wa Diego kujaribu kumpiga kichwa David Luiz.

Maxwell appeals to the ref as David Luiz reacts to a confrontation with Diego Costa

PSG wanaelekea kwenye uwanja wa Stamford Bridge hii leo huku wakijua umuhimu wa ushindi wa mabao mawili kwa moja waliouchuma katika uwanja wao wa nyumbani majuma mawili yaliyopita, hivyo itawalazimu kuulinda kwa hali yoyote ile.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza mabao ya PSG yalifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Sweden, Zlatan Ibrahimović pamoja na Edinson Roberto Cavani Gómez, kutoka nchini Uruguay huku bao la kufutia machozi la Chelsea likifungwa na John Obi Mikel.

Mkwasa Atangaza Kikosi Cha Taifa Stars
Real Madird Kusaka Heshima Barani Ulaya Leo