Bondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuhudhuria pambano lake dhidi ya bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eric Katompa.

Awali pambano hilo lilikuwa lifanyike Juni 24 mkoani Dodoma lakini lilisogezwa mbele na sasa litafanyika usiku wa Julai 15 jijini Dar es Salaam.

Dulla Mbabe amesema Dar es salaam kuwa anatamani kumuona Rais Samia Suluhu Hassan kwenye pambano hilo kama mgeni rasmi kwani anaamini ni siku atakayolitangaza taifa kwenye mchezo wa ngumi.

“Nataka kurejesha heshima yangu lakini pia kulitangaza taifa la Tanzania kupitia mchezo huu, ndio maana natamani Rais Samia awe mgeni rasmi,” amesema Pazi

Hii ni mara ya pili mabondia hao wanakwenda kukutana baada ya mwaka juzi (2021) kupambana, ambapo Katompa alimfumua Dulla Mbabe.

Ruto awashutumu watendaji KRA kwa rushwa
Minziro: Sifahamu kinachoendelea Geita Gold