Mweusi G- Nako ameanza kusakwa na wasanii mbalimbali wa Kimataifa baada ya video ya wimbo wake O-G kuanza kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga vya kimataifa ikiwemo MTV.

Akiongea na E-News ya Channel 5, Warawara amesema kuwa ameanza kupata mialiko ya collabo kutoka kwa wasanii mbalimbali wa kimataifa na wengi wamevutiwa na namna ambavyo ameweza kuflow kwenye mdundo wenye mapigo ya kiasili.

Rapa huyo amewashauri wasanii wenzake kuvitumia vionjo vya kiafrika kufanya ngoma zao kuwa ‘Orijino’ na kupata utambulisho kama ilivyo kwa nyimbo za Afrika Magharibi na Afrika Kusini.

 

Ali Kiba: Usinifananishe na Msanii yeyote Tanzania
TFF Yaonya Upangaji Wa Matokeo