Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Stephen Mhando ameibuka mshindi wa Tuzo ya Afisa Uhusiano Bora kwa mwaka 2022 kwenye sekta ya madini.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Stephen Mhando.

Tuzo hizo za umahiri zilitolewa Februari 18, 2023 jijini Dar es Salaam na Chama cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) zinaifanya Kampuni hiyo kuendelea kufanya vyema kwenye nyanja mbalimbali zinazogusa jamii na serikali kwa ujumla.

Mbali na Mhando, GGML pia iliibuka mshindi wa pili katika tuzo ya taasisi bora inayowajibikaji kwa Jamii (CSR), ambapo kwa pamoja zilipokewa na Mhando.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Mhando aliwashukuru wadau mbalimbali ikiwamo wale anaofanya nao kazi hasa ikizingatiwa kwa asilimia kubwa ndio wamemuwezesha kuibuka mshindi na kuwa kati ya maofisa uhusiano nguli nchini kwenye sekta ya madini.

Tuzo hizo ambazo zimetolewa kwa mara ya kwanza na PRST, zinalenga kukuza na kuhamasisha ubora wa kitaaluma, ubunifu katika kupanga, kutetea, kushawishi, kutekeleza na kupima majukumu ya maofisa uhusiano katika maeneo yao ya kazi.

Waziri atoa maagizo kwa kamati za ulinzi na usalama NEMC
Mangungu: Waandishi wa Habari mnachochea