Gwiji wa soka duniani Johan Cruyff, amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu.

Taarifa iliyotolewana familia ya gwiji huyo kutoka nchini Uholanzi, imeeleza kwamba baba yao amefikwa na umauti hii leo baada ya kuugua kwa muda mrefu kansa ya mapafu.

Cruyff amafariki dunia akiwa na umri wa miaka 68, na ataendelea kukumbukwa kufuatia mchango wake alioutoa katika soka la nchini Uholanzi pamoja na baadhi ya klabu za barani Ulaya na Marekani.

Klabu ambazo aliwahi kuzitumikia ni Ajax (1964–1973), Barcelona (1973–1978) Los Angeles Aztecs (1979–1980) Washington Diplomats (1980–1981), Levante (1981), Ajax (1981–1983) na Feyenoord (1983–1984).

Kwa upande wa timu ya taifa ya Uholanzi Cruyff ameitumikia kuanzia mwaka 1966 hadi 1977 katika michezo 48 na kufunga mabao 33.

Johan Cruyff ndie muanzilishi wa mfumo wa soka wa Total Football (mchezo wa kumiliki mpira) ambao aliutambulisha alipokua meneja wa FC Barcelona kati ya mwaka 1988–1996.

Klabu nyingine alizowahi kuzifundisha ni Ajax ya nchini kwao Uholanzi kuanzia mwaka 1985 hadi 1988 na Catalonia ya nchini Hispania kuanzia mwaka 2009 hadi 2013.

Takukuru wakomaa na Zitto, Bashe... Bashe ashtukia kitu
Man City Waanza Kutii Maagizo Ya Guardiola