Beki kutoka nchini Zambia, Stoppila Sunzu amerejea nchini Ufaransa kujiunga na klabu ya Lille kwa mkataba wa mkopo akitokea nchini China katika klabu ya Shanghai Shenhua.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, atajiunga na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia, Herve Renard kwa mara ya tatu tangu walipojuana mwaka 2008 kwenye kikosi cha Chipolopolo.

Herve Renard, ndiye alimpeleka Sunzu, nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza, baada ya kuachana na timu ya taifa ya Zambia na kwenda kukinoa kikosi cha klabu ya Sochaux katika msimu wa 2013-14.

Sunzu ambaye pia waliwahi kuitumikia klabu ya TP MAzembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesema ni hatua nzuri kwake kuelekea nchini Ufaransa kucheza soka, na anaamini mambo yatakuwa mazuri sana kwake pamoja na klabu ya Lille iliyomsajili kwa mkopo.

Beki huyo ameongeza kuwa kufanya kazi tena na kocha Herve Renard, pia kumemfurahisha kutokana na ukaribu uliopo kati yake na kocha huyo kutoka nchini Ufaransa.

Wawili hao walikuwa chachu kwa taifa ya Zambia mwaka 2012, baada ya kuiwezesha timu ya taifa ya nchi hiyo kutwaa ubingwa wa barani Afrika kwa kuibanjua Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Zokora Kumalizia Soka Lake Ligi Kuu Ya India
Joto Urais FIFA : Prince Ali Ampinga Platini