Uongozi wa chama cha soka nchini Wales (FAW), kimepingana na ombi la klabu ya Hull City ya nchini England, la kuhitaji kumuajiri kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Chris Coleman.

Taarifa iliyotolewa na FAW imeeleza kuwa, ni vigumu kwa sasa kocha huyo kuondoka kutokana na mipango mizuri iliyowekwa nchini humo kwa ajili ya kuiwezesha timu ya taifa ya Wales kufanya vizuri zaidi ya ilivyokua kwenye fainali za Euro 2016.

Coleman, alikiongoza kikosi cha Wales hadi katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 na sasa anatarajiwa kufanya kazi yake ipasavyo kwa kuipeleka nchi hiyo kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi.

Uongozi wa klabu ya Hull City ulikua umeonyesha nia ya kutaka kuvunja mkataba wa kocha huyo ambao umesaliwa na muda wa miaka miwili.

Kushindikana kwa mpango huo, Hull City wameanza kumfikiria Gianfranco Zola ama Roberto Martinez ili kujaza nafasi ya Steve Bruce aliyetangaza kujiuzulu.

Video: Basata wakanusha kumalizana na Msanii Nay wa Mitego
Paul Pogba Aupa Kisogo Usajili Wa Pauni Milioni 100