Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), imeitaka jamii na sekta zinazojishughulisha na mazingira kuchukua tahadhari ya mafuriko

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Dkt. Agnes Kijazi ambapo amesema kuwa katika miezi hiyo kunatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa zitakazosababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo.

“Wadau wa sekta ya uvuvi, kilimo, mifugo, chakula na wanyamapori wanatakiwa kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya hewa. Kufahamu mapema kutasaidia kujipanga na kujikinga na majanga ambayo yanaweza kusababisha mafuriko.”amesema Kijazi

Amesema katika msimu huo, hali ya unyevunyevu ardhini inatarajia  kuwa ya kuridhisha katika maeneo mengi hapa nchini, hivyo jamii inatakiwa ichukue tahadhari kubwa ili kuweza kujikinga na mafuriko.

Hata hivyo, Dkt. Kijazi ameongeza kuwa katika kipindi hicho kifupi cha mvua wachimbaji wadogo wa madini wanapaswa kuwa makini kwa kuwa ongezeko la maji kwenye udongo linaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi na kuleta maafa

Wanawake 28 wahitimu kozi ya ukocha TFF
Lulu kupandishwa tena kizimbani