Mlinda mlango wa Man City Joe Hart hii leo anatarajiwa kusafiri hadi mjini Turin nchini Italia, kwa ajili ya kufanyia vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wa mkopo katika klabu ya Torino.

Hart jana alikua miongoni mwa wachezaji walioripoti kwenye kambi ya timu ya taifa ya England huko George’s Park, lakini saa kadhaa baadae taarifa iliyotolewa na chama cha soka FA, ilithibitisha safari ya mlinda mlango huyo ambae amewekwa pembeni na meneja mpya wa Man City Pep Guardiola.

Hart mwenye umri wa miaka 29, ameshindwa kumshawishi meneja huyo kutoka nchini Hispania kutokana na kuwa na mfumo tofauti wa uchezaji ambao umekua haumpendezi Guardiola ambaye anadai hupendelea kuwa na mlinda mlango anaeanzisha mashambilizi.

Tayari klabu ya Man City imeshamsajili mlinda mlango wa Chile Claudio Bravo akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona, na anaaminiwa ataenda sambamba na mfumo unaotumiwa na Guardiola.

Kwa mara ya mwisho Hart aliitumikia Man City katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya mtoano ya michuano ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Steaua Bucharest katikati ya juma lililopita, lakini ilikua ngumu kwake kucheza katika michezo mitatu ya ligi ya England ambapo mara zote alianzishwa Willy Caballero.

Wakala wa Hart, Jonathan Barnett amekaririwa na tovuti ya www.tuttosport.com akisema  “Ndio, Joe Hart ataitumikia Torino. Na tayari mambo yote yanakwenda vizuri. Mchezaji ameshakubaliana na uongozi wa klabu yake (Manchester City) na kesho (leo) ataelekea nchini Italia kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Mpango wa usajili wa mkopo wa kujiunga na klabu ya Torino utakua suluhisho kwa Joe Hart la kucheza katika kikosi cha kwanza ili asipoteze nafasi yake kwenye timu ya taifa ya England.

Kwa upande wa mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Torino, Gianluca Petrachi amesema wanafurahishwa na mpango wa kumpata mlinda mlango huyo, kutokana na hitaji lao kusimamia kwenye nafasi hiyo.

Klabu ya Torino, ilimaliza msimu uliopita wa ligi ya Sirie A, ikiwa katika nafasi ya 12, na tayari imeshajikusanyia point tatu katika michezo miwili waliyocheza tangu mwanzoni mwa msimu huu.

Nacer Chadli Ailazimisha West Brom Kuvunja Benki
Arsenal Yamuweka Sokoni Jack Wilshere Kwa Masharti