Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), linatarajia kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwake, kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini Septemba 1 mwaka huu.

Msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema kuwa jeshi hilo litasherehekea bila kufanya maandamano ya aina yoyote na kwamba linafahamu Serikali imeshapiga marufuku maandamano siku hiyo.

“Ratiba yetu ni kusherehekea, tunajua Serikali imeshakataza maandamano,” alisema Kanali Ngemela. “Sisi wanajeshi tukipanga shughuli zetu zinakwenda kama zilivyopangwa,” aliongeza.

JWTZ liliundwa Septemba mwaka 1964 baada ya kuvunjwa rasmi kwa jeshi lililorithiwa kutoka kwa wakololini la Tanganyika Rifles.

Tamko hilo la JWTZ limekuja wakati ambapo kumekuwa na mvutano wa kufanyika kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA ya Chadema ambayo Serikali imeyapiga marufuku.

Waziri aagiza Machinga waondolewe Kariakoo, ‘asema Rais hakumaanisha warudi’
Ccm Wampongeza Raisi Magufuli Na Serikali Yake Kwa Mafanikio Aliyoyapata Kwa Muda Mfupi