Serikali imesema kuna ongezeko la wagonjwa wa wapya wa saratani wapatao 50,000 nchini na inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na ogezeko la asilimia 50 ya wagonjwa wapya.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na watoto, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa uzinduzi wa idara ya magonjwa ya saratani, huduma za patholojia kwenye Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Gwajima amesema kuwa saratani inashika nafasi ya tano kwa kusababisha vifo kwa wanaume na nafasi ya pili kwa wanawake kwa mujibu wa takwimu za vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza nchini.

Saratani zinazoongoza kwa wanawake ni mlango wa kizazi na saratani ya matiti, huku kwa upande wa wanaume saratani za tezi dume, koo, kichwa pamoja na shingo zikiongoza.

Aidha, Waziri Gwajima ametoa rai kwa wananchi kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara, kwani asilimia 75 ya wagonjwa wa saratani wanafika hospitali wakiwa katika hatua ya mwisho jambo linalosababisha ugumu kwa madaktari kuwatibu.

Young Africans kuanza kambi Januari 25
Boeing 737 Max kurejea tena anga la Ulaya