Kivumbi cha Uchaguzi kinatarajiwa kutimka Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu jimbo hilo kuwa liko wazi na kwamba linaweza kuitisha uchaguzi.

Hatua ya Spika kutangaza kuwa Jimbo la Singida Kaskazini liko wazi imetokana na aliyekuwa mbunge eneo hilo, Lazaro Nyalandu kutangaza kujiuzulu uanachama wa CCM na ubunge.

Taarifa iliyotolewa na Bunge imesema kuwa Jimbo hilo limekuwa wazi tangu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo, Lazaro Nyalandu kufutwa uanachama na chama chake cha CCM, Oktoba 30 mwaka huu.

“Kufuatia taarifa hiyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge atakaye jaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi ya Jimbo la Singida Kaskazini,”imesema taarifa hiyo

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliandika barua hiyo kwa mujibu wa kifungu 37(3) cha sheria ya NEC (Sura ya 343, ya mwaka 2015).

Chadema: Tunauhakika tutashinda jimboni kwa Nyalandu
Video: Nape amshukia Nyalandu, Wabunge kikaangoni