Serikali imeiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa juu ya sakata la mechi ya watani wa jadi  timu za Simba na Yanga uliokuwa uchezwe katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Mei 8 2021.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kipindi cha kutambulisha wageni waliotembelea Bunge leo Jumatatu Mei 10 2021.

Amesema baada ya kuahirishwa wa mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga uliotakiwa kuchezwa Mei 8 mwaka huu kulisababisha manung’uniko katika mitandao ya jamii lakini pia kutojua hatima ya waliolipa kiingilio katika mchezo huo kumezua sintofahamu.

Amesema tukio hilo limevuta hisia Kwa Watanzania ndani na nje kwa sababu  timu hizi ndizo zimebeba taswira ya mpira wa miguu Tanzania.

“Kufuatia kero hii  tayari tumeagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha inatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania,  mchezo wenyewe utachezwa lini lakini kuna viingilio ambavyo walikuwa wametoa mashabiki hatima yake nini,” amesema.

Amesema wizara hiyo inatakiwa kutoa taarifa hiyo kwa kushirikiana na chombo kinachosimamia mchezo huo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

“Naomba kuwasihi Watanzania hasa wapenzi wa michezo kwenye eneo la mpira wa miguu ambao walijiandaa kusikia na kuangalia mpira wa miguu, tuipe muda wizara itoe taarifa kwa kushirikiana na taasisi inayoshughulikia mpira wa miguu,” amesema.

Sudan Kusini: Rais Salva Kiir avunja Bunge
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 10, 2021