Majogoo wa jiji Liverpool, wameshindwa kufurukuta mbele ya AS Roma katika mchezo wa michuano ya International Champions Cup uliochezwa nchini Marekani mapema hii leo.

Liverpool wamekubali kibano cha mabao mawili kwa moja, ikiwa ni sehemu ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini England ambao utaanza rasmi mwishoni mwa juma lijalo.

Mabao ya AS Roma yalipachikwa wavuni na Edin Dzeko pamoja na Mohamed Salah huku lile la Liverpool likifungwa na kinda, Sheyi Ojo.

Meneja wa The Reds, Jurgen Klopp alijaribu kupanga kikosi cha nguvu katika mchezo huo kwa kuwaanzisha washambuliaji Sadio Mane, Georginio Wijnaldum pamoja na Daniel Sturridge, lakini bado majogoo ya jiji yalishindwa kufurukuta.

Alex Song Atimkia Urusi
Donald Trump afyatuka, adai Clinton ni ‘Shetani’