Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameanza kuishi kauli zake alizozitoa wakati akifanya mahojiano maalum na kituo cha BBC.

Lowassa ametumia kipindi cha mapumziko kutembelea mradi wake wa ufugaji ng’ombe ulioko Handeni jijini Tanga na kuanza kuwachunga ng’ombe wake kama wafanyavyo wafugaji wengine waishio katika maeneo ya machungani.

Lowassa na Ng'ombe 3

Lowassa ameonekana katika picha akiwa na mlinzi wake akiongoza kundi kubwa la ng’ombe wake kuelekea malishoni.

Lowassa na Ng'ombe 2

Katika hatua nyingine, Lowassa na familia yake walishiriki ibada katika kanisa la KKKT wilayani Handeni. Akiwa katika kanisa hilo, alipewa nafasi ya kuzungumza ambapo aliwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwa kuwa na imani naye. Aliwataka wananchi wote kudumisha amani, upendo na utulivu.

Lowassa ambaye pia ni waziri Mkuu mstaafu aliwataka wananchi wote kudumisha amani na utulivu kwani ndio silaha ya maendeleo.

Kasi ya Magufuli Kumpitia Sumaye na Boss wa S.H Amon
Ben Pol Amuomba Radhi Ali Kiba