Beki wa kushoto wa Man Utd, Luke Shaw hii leo ataendelea kufanyiwa matibabu mjini Eindhovein baada ya kupasuliwa kwa mara ya kwanza usiku wa kuamkia jana.

Taarifa kutoka Old Trafford zinaelza, Shaw atafanyiwa upasuaji mwingine hii leo katika hospitali ya St Anna Ziekenhuis.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 20, alivunjika mguu baada ya kukabiliwa na beki wa PSV Eindhoven, Hector Moreno wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa siku ya jumanne.

Shaw, alipata majeraha ya kuvunjika mguu katika dakika ya 15 ya mchezo huo.

Tayari familia ya Luke Shaw imeshajiunga nae huko nchini Uholanzi kwa ajili ya kumfariji katika kipindi hiki kigumu kwake, ambapo itashuhudiwa akiwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita ijayo.

Bolt Aikumbuka Shule Iliyompa Elimu
Jerome Valcke Asimamishwa Kazi FIFA