Kesi inayomkabili muigizaji wa Filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo alhamisi imeendelea kusikilizwa Mahakamani ambapo washauri watatu wa Mahakama kuu wamesema mshitakiwa Lulu aliua bila ya kukusudia.

Baada ya kusikiliza maoni ya baraza la wazee leo Mahakama kuu ya tanzania, imesema Elizabeth Michael amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia, muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake na hukumu yake itatolewa Novemba 13.

Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.

Kabla ya  wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa.

Jaji Warioba awafunda wanasiasa
Askari wawili FFU kikaangoni kwa kupiga raia