Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango amewaasa Wakuu wa Mikoa kusimamia uchumi wa Mikoa waliyopangiwa kwa tija ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na wa mwananchi kwa ujumla

Ameyasema hayo leo Mei 19, 2021 wakati wa uapisho wa Wakuu wa Mikoa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu kwa viongozi hao.

Mpango amesema kuwa moja ya sifa ya kiongozi ni kuwa hodari na kuwa mfano kwenye kazi, akiongeza kuwa kama viongozi ni vyema wakajua matatizo ya wananchi na kuyatatua.

”Kiongozi mzuri ni lazima awe na sifa mbili, Hodari wa kazi na awe mfano kwa tabia, viongozi ambao mmepewa dhamana leo na wale waliopo ni muhimu sana tusiende kwenye vituo vyetu vya kazi tukawa mfano mbaya na tusichape kazi kwenye nchi masikini kama yetu,” amesema Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango amewaasa viongozi hao kushugulikia wazembe, wabadhirifu, wasio na nidhamu na kuwataka kutenda haki.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 20, 2021
Kocha Hunt aihofia Simba SC kwa Mkapa