Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaonya Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutojihusisha na migogoro ya ardhi na atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Ameyasema hayo leo Juni 2, 2021 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa aliowateua hivi karibuni.

“Sita vumilia kusikia , Mkuu wa Mkoa kajiingiza kwenye mgogoro wa ardhi kaingia kwenye Mkoa wa watu kakuta ardhi kajimilikisha anaitumia yeye anaacha watu wanalalamika”. Amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia amewataka kuhakikisha wanasimamia vyema matumizi mazuri ya serikali kwa kusimamia miradi ya serikali kwenye mikoa yao iendane na thamani ya fedha inayutumia.

Sio mpaka Rais afike pale akasimame na kuhesabu mabati, matofali aone kwamba yanaendana na thamani yaa pesa iliyotajwa, Hayati Rais Magufuli alikuwa na huo ujuzi wa kwenda na kuhesabu mabati, matofali Rais mimi sina huo ujuzi”. Amesema Rais Samia.

Sambamba na hayo pia amewahasa voingozi hao aliowaapisha wakasimamie vizuri sekta ya utumish wa umma kwenye mikoa kwa kutenda haki upandishaji wa vyeo bila upendeleo na kuhakikisha wanakomesha tabia iliyopo ya kuhamisha wafanyakazi bila mpangilio.

Hali kadhalika Rais Samia amewahasa wakasimamie uchumi wa viwanda kwenye mikoa yao kwa kutenga mazingira rafiki kwa wawekezaji watakapokuja kuekeza katika maeneo yao.

Tanzania kuja na kilimo cha Tija
Jenerali wa Uganda aliyepigwa risasi azungumza